Wednesday, 3 August 2016

Siyo kila kizuri na kitamu ni salama kwa afya yako. Hebu jifunze hapa leo


Je, vyakula vitamuvitamu mfano keki,biskuti, chipsi, kuku wa kukaangwa na vingine vingi vyenye kufanana na hivyo vinamanufaa gani kwa afya zetu?

Naomba leo nikwambie kwamba usitegemee mwili wako kama utaweza kuwa katika hali nzuri ya kiafya kwa kuvitegemea vyakula vya aina hiyo pekee.

Pamoja na hayo napenda ufahamu kuwa vyakula vyenye manufaa mwilini ni pamoja na matunda, mbogamboga, mayai na njugu.

Acha kupenda vyakula vya kuiva harakaharaka vinavyofanya maisha yetu kuwa rahisi kwa sababu tunavipika haraka haraka na kwa urahisi, lakini lazima tutambue kuwa vyakula hivyo vina mafuta mengi na havina virutubisho vya kutosha.

Vyakula vilivyowekwa kwenye jokofu, vilivyohifadhiwa ndani ya makaratasi na mikebe si rafiki sana kwa afya zetu.

Kumbuka kuwa kula vizuri kunahusu kufanya uamuzi unaofaa kila mara. Lengo lako liwe tu kula lishe bora zenye virutubisho vyote visivyo na mafuta mengi na ambavyo si vya kunonesha.

Kama unapenda kufahamu zaidi kuhusu vyakula vyenye virutubisho nzuri mwilini mwako unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment