Thursday, 11 August 2016

Tumia vyakula hivi ili kuepuka maumivu ya mwiliKwa wewe unayesumbuliwa na maumivu mbalimbali mwilini kila mara fanya yafuatayo kwa muda wa wiki 2 au mpaka utakapopona kabisa;

1. Matunda
Jitahidi kula matunda, unaweza ukaamua moja kati ya milo yako iwe ni matunda tu, mfano unaweza ukaamua kula chakula cha mchana au cha usiku, lakini ukahakikisha mlo wako unamatunda yakutosha.

2. Mboga za majani
 Hakikisha mlo wako unamjumuiko wa mboga za majani unaweza kula vyakula vingine kama samaki wa kukaangwa au nyama ya kukaangwa, pembeni weka sahani iliyojaa mboga majani, kula hivyo 

3. Chai ya tangawizi
 Chemsha chai ya kutosha ya tangawizi angalau kikombe kimoja kila siku kisha kunywa chai hiyo bila kuchanganywa na majani.

4.Maji
Kunywa maji glasi 8 hadi 10 kila siku.

6. Mazoezi,
Mazoezi ni muhimu sana kiafya na husaidia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali pamoja na kuufanya mwili kuwa mchangamfu.

Unaweza kupata ushauri zaidi chini ya taasisi ya The Work Up Tanzania (WUTA) kuhusu masuala ya mazoezi na masuala ya lishe bora tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandait@gmail.com


.

No comments:

Post a Comment