Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 30 August 2016

Ukiona dalili hizi 5 waone wataalam kwani huashiria afya yako haipo sawa


Kuna wakati unaweza kujikuta hauko vizuri kila siku na ukashindwa kujua nini tatizo.

Sasa leo napenda tujuzane hizi dalili ambazo ikiwa utaziona basi huenda ukawa na matatizo kiafya:-

Mabadiliko ya ngozi.
Ngozi ni alama tosha ambayo huashiria uwepo wa afya bora kwa binadamu hivyo basi ikiwa utaona ngozi yako imeanza kupoteza uhalisia wake basi ujue huenda tayari kunatatizo la kiafya linakunyemelea hivyo unaweza kuwaona wataalam kwa ushauri zaidi.

Mabadiliko ya njoo.
Unapoona kuanza mabadiliko ya haja ndogo au haja kubwa basi huenda nayo ikawa dalili ya tatizo, hivyo ni vyema kuwa mchunguzaji wa haja zako ili kung'amua baadhi ya matatizo ya kiafya kwa haraka na kuyatafutia ufumbuzi kwa wataalam.

Matatizo ya kukosa usingizi.
Hii nayo huweza kuwa ni kiashiria cha tatizo mwilini mwako hivyo unapoona mabadiliko yanahusu usingizi pia unaweza kujichunguza vizuri na unapoona huelewi basi waone wataalam kwa ufafanuzi zaidi.

Midomo kukauka.
Unapoona midomo inakauka au kupasuka nayo huweza kuwa dalili mbaya kiafya hivyo unaweza kufanya maamuzi ya kwenda kufanya uchunguzi wa kiafya ili kujua tatizo zaidi.

Mabadiliko ya joto la mwili
Iwapo mwili unakuwa na joto mara kwa mara nayo huweza kuwa ni moja ya kiashiria cha tatizo kiafya, hivyo ni vyema kuwaona wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment