Wednesday, 10 August 2016

WUTA inakuletea ushauri wa namna ya kujiepusha na U.T.I


U.T.I ni kifupi cha maneno ya kingereza ikiwa na maana  ‘Urinary Tract Infections’ ambayo  ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. 

Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na tatizo hilo.

Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

1. Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.

2. Jitahidi kuwa msafi

3. Mara zote jisafishe kutoka mbele kurudi nyuma na jitahidi kuepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
.
4. Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.

5. Usikae na mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda ukfanye hivyo.

6. Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.

7. Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.

Ushauri huu umetolewa na shirika liliso lakiserikali liitwalo The Work Up Tanzania (WUTA) unaweza kuwasiliana nao zaidi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment