Sunday, 21 August 2016

Yafahamu haya mambo 7 muhimu ya kiafya kuhusu pilipili hoho

Pilipili hoho unaweza kuiweka kwenye kundi la mbogamboga, lakini pia si vibaya ukiweka hata kwenye kundi la viungo ambacho huweza kuliwa baada ya kupikwa au hata ikiwa mbichi hususani kwenye kachumbari.

Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana ndani ya hoho ni pamoja na vitamin C pamoja na collagen ambayo husaidia kulinda afya ya ngozi, lakini pia vitamin C husaidia kujenga kinga za mwili.

Aidha, ndani ya hoho pia kuna madini mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini ya chuma, calcium, copper, magnesium, zinc  pamoja na kiwango kidogo cha selenium.

Hoho pia ina kiwango cha 'fiber', hivyo husaidia kuboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Mbali na hayo, hoho pia husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants' ambacho husaidia kushusha kiwango cha cholesterol mwilini.

Hoho ni kiungo kizuri kwa wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito wa mwili kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha 'calorie'.

Hupunguza uwezekano wa matatizo ya mfumo wa hewa, hii ni kutokana na kuwa na utajiri  wa vitamin C pamoja na 'antioxidants'  ambavyo husaidia kurekebisha mfumo wa upumuaji.

Huimarisha kinga za mwili, hii ni kutokana na kuwa na kiwango cha vitamin C ambayo kwa kiasi kikubwa hufanya kazi ya kuboresha kinga za mwili ndani ya miili yetu.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambali linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.
 


No comments:

Post a Comment