Thursday, 4 August 2016

Zipo hapa mbinu za kuongeza uwezo wa kumbukumbu zako


Mara nyingi watu wengi wanapozidi kukua hujikuta wakianza kukumbwa na baadhi ya mabadiliko ikiwa ni pamoja na suala la kupoteza kumbukumbu.

Baadhi yao hujikuta wamefika sehemu fulani halafu wamesahau ni kwanini wamefika sehemu hiyo.

Tatizo hili huweza kumkumba mtu yoyote katika maisha yake, lakini zaidi wale wenye umri mkubwa.

Matatizo mengi ya kupoteza kumbukumbu huonesha mabadiliko katika muundo na ufanyaji kazi wa ubongo.

Punguza mzigo kwenye ubongo wako.
Ni vyema ukapunguza baadhi ya mambo akili mwako na badala yake jifunze mambo mengine mapya na yaliyomuhimu.

Tunza vitu vyako sehemu yenye kuoneana kirahisi ili kuirahisishia akili yako kufikiria. Kama upo ofisini jaribu kupunguza vitu visivyohitajika ili uwe karibu na vitu unavyohitaji kuvitumia tu.

Rudia kile unachohitaji kukijua zaidi
Ukihitaji kukumbuka kitu ulichosikia au kusoma basi jitahidi kukirudia mara kwa mara kadri uwezavyo. Kitendo cha kufanya hivyo utakuwa unaimarisha kumbukumbu yako.

Kujiamini
Unapokosa kujiamini na kuhisi kweli wewe huna kumbukumbu basi dhana hii kuna wakati huweza kuwa kweli hivyo ni vyema ukajiamini kwa kila jambo. Wengi wetu huwa tunaamini kadri tunavyozeeka ndivyo tunapoteza kumbukumbu hivyo ni vyema tukaondoa dhana hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo.

Kwa ushauri zaidi kuhusu masuala mbalimbali unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gamial.com

No comments:

Post a Comment