Saturday, 13 August 2016

Zipo hapa sifa za mafuta ya nazi na namna ya kuyaandaa ukiwa nyumbani

Mafuta ya nazi ni mazuri kiafya endapo yatatumika vizuri kwani yamekuwa yakisifika kwa kuimarisha afya ya ngozi na kuboresha muonekano mzuri.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za matumizi ya mafuta hayo.

Hung'arisha ngozi
Kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako.

Mafuta hayo pia yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi.

Husaidia kukuza nywele
Unapotumia mafuta ya nazi kwenye nywele husaidia kuzifanya nywele zako kukua kwa haraka na kuzifanya kuonekana zenye afya  na zenye kung'aa, lakini pia mafuta haya husaidia kuondoa mba kwenye nywele.


Hutumika kulainisha sehemu za siri
Wanawake wenye tatizo la ukavu sehemu za siri huweza kupata ahueni kwa kutumia mafuta hayo  ya nazi .

Ipate hii video ya namna ya kuandaa mafuta ya nazi hapa chini
 
Ushauri huu umetolewa na shirika liliso la kiserikali liitwalo The Work Up Tanzania (WUTA) unaweza kuwasiliana nasi zaidi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:

Post a Comment