Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 1 September 2016

Fahamu namna ya kutumia vizuri kiungo cha mdalasini

Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji hususani chai.

Mdalasini unaweza kutumika kuanzia magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani.

Unapotumia unga wa magome yake huweza kupunguza uwezekano wa magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni.

Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi.
Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini

Pia mdalasini na asali husaidia kupunguza uwezekano wa kukumbwa na mafua pamoja na kikohozi

Mbali na hayo pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa au kutuliza tatizo la gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa.

Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya lishe bora.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment