Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 27 September 2016

Faida 3 utakazopata kwa kula 'apple' kwa wiki 1 mfululizo

Mungu ametujalia matunda ya aina mbalimbali na karibu kila matunda huwa na manufaa kiafya husani pale yanapotumika vizuri.

Hapa ninazo dondoo muhimu za tunda la tufaa au 'apple'

Kwanza napenda msomaji wangu utambue kuwa unapokula tunda hili  fahamu kuwa unakuwa na nafasi nzuri ya kuepuka matatizo ya ukosefu wa choo pamoja na maumivu ya tumbo ya hapa na pale kwani tunda hili lina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambayo husaidia kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Aidha, ulaji wa apple pia husaidia kumlinda mlaji wa tunda hilo dhidi ya matatizo ya ya moyo pamoja na uzio au 'allergy reaction'   .

Kama hiyo haitoshi napenda ufahamu kuwa kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa na St George's Hospital Medical School iliyopo London walibaini kuwa watu ambao hula maaple matano au zaidi kwa wiki huwa na afya nzuri ya mapafu kuliko wale ambao hawatumii tunda hilo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.No comments:

Post a Comment