Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 6 September 2016

Fanya mambo haya 7 kila siku ili uendelee kuwa na afya bora


Kila mtu hupenda kuwa na afya njema wakati wote ili kuweza kuendelea na mikakati ya kila siku ya kuendesha maisha.

Hapa ninazo baadhi ya kanuni ambazo zikifuatwa vizuri huweza kukusaidia kuwa na afya njema siku zote.

Hewa safi
Hewa safi ni muhimu wakati wote iwe mchana au usiku, hivyo hakikisha nyumba yako au mahali pako pa kazi kuna mazingira ambayo yanaruhusu uwepo wa hewa safi muda wote.Hewa safi husaidia damu kuzunguka vizuri mwilini kutokana na kuwa na kiwango cha kutosha cha oksijeni.

Kupata muda wa kupumzika
Kwa kawaida mwili ni muhimu kupumzika kutokana na msongo wa majukumu ya kila siku

Mazoezi
Mazoezi nayo ni muhimu sana kwa afya zetu ikiwa ni pamoja na kuulinda mwili dhidi ya magonjwa yasiyoyakuambukiza, pia mazoezi husaidia kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri ndani ya mwili pamoja na kukufanya kuwa na uwezo mzuri na wa haraka katika kufanya maamuzi.

Maji
Inatupaswa kunywa maji ya kutosha kutokana na maji kuwa na umuhimu mkubwa kwa kila seli ndani ya mwili. Karibia asilimia 70 ya miili yetu ni maji hivyo inaonesha ni kwa kiasi gani maji yanaumuhimu kwa afya zetu.

Lishe bora.
Wataalam wa lishe bora wamekuwa wakishauri matumizi ya chakula cha awali yaani nafaka, kokwa, matunda na mbogamboga. Ukitaka kuanza kula vyakula vya mimea hakikisha unafahamu vizuri namna ya kuandaa lishe bora.

Epuka vitu vyenye madhara
Mfano wa vitu hivyo ni sigara, dawa za kulevya pombe nk.Ni vyema ukatambua kuwa matumizi ya pombe huathiri mfumo mzima wa kinga za mwili na kuufanya kuwa dhaifu.Pia huchangia kudhoofisha mfumo mzima wa uzazi kwa jinsia zote mbili.

Kumuamini Mungu
Watu wengi wambao husimama katika imani zao Mungu huwasaidia na kulinda afya zao mara zote.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.No comments:

Post a Comment