Sunday, 18 September 2016

Hii hapa mbinu rahisi za kumaliza tatizo la chunusi


Tatizo la chunusi ni moja ya matatizo ambayo huwasumbua vijana wengi wakike na wa kiume, lakini pia huwakosesha raha pia.

Leo ninazo hizi mbinu za kukabiliana na tatizo hilo kama ifuatavyo:-

Nawa uso kwa maji na sabuni kila siku jioni na asubuhi. Pia usikubali kulala usiku bila kusafisha uso au kuoga. Hii itasaidia kuondoa mafuta kwenye ngozi na kupunguza bakteria wanaoshambulia na kusababisha uvimbe wa chunusi.

Epuka kukamua chunusi ambazo hazijaiva, pia usizishikeshike ili kuepuka makovu meusi usoni na kuepuka kuvimbe uso.

Epuka kutumia vipodozi vyenye mafuta hasa katika sehemu zenye kuathiriwa na chunusi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment