Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 8 September 2016

Hivi ndio vyakula ambavyo huweza kuwasaida wanawake wenye uzazi wa mbali kuwa karibuKupata mtoto ni moja ya jambo muhimu na la furaha katika familia yoyote, licha ya kwamba kwa baadhi ya wanafamilia jambo hili limekuwa changamoto kwao.

Leo ninayo orodha ya vyakula ambavyo huweza kusaidia kuweka uzazi kuwa wakaribu zaidi.

Mayai
Mayai yamesheheni virutubisho vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin D ambayo husaidia kuhamasisha uzazi kuwa karibu. Kwa mujibu wa utafiti uliowahikufanywa katika chuo cha Yale University ambapo walibaini kuwa wanawake wenye upungufu wa vitamin D huweza kupatwa na changamoto ya uzazi.

Samaki
salmon
Samaki nao husogeza karibu uzazi kwa wale wenye uzazi wa mbali kutokana na kitoweo hicho kuwa na kirutubisho cha omega 3 ambayo husaidia kurekebisha homoni za masuala ya uzazi ndani ya mwili, lakini pia huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye viungo vya uzazi.

Parachichi

Hili ni tunda muhimu pia kwa masuala ya uzazi kutokana na kuwa na virutubisho vya folic acid, monounsaturated fat pamoja na vitamin B ambazo kwa pamoja husaidia kuamsha homoni za uzazi kwa wanawake na wanaume.

Monounsaturated fat ambayo hupatika kwenye parachichi husaidia kurekebisha homoni ambazo husimamia masuala ya uzazi ndani ya mwili na hivyo kuongeza uwezekano wa kushika ujauzito kirahisi zaidi.

Broccol
Hii ni aina ya mbogamboga ambayo ndani yake imesheheni kiwango kikubwa cha vitamin C ambapo vitamini hiyo ni miongoni mwa vitu muhimu kwenye suala ya uzazi kwani husaida mwanaume kuwa na manii yenye uwezo wa kutungisha mimba , lakini kwa wanawake huweza kusaidia kutoharibika kwa mimba mara kwa mara.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment