Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 11 September 2016

Hizi hapa siri 5 za kuepuka tatizo la kuota kijinyama sehemu ya haja kubwa, maji nayo yanahusika

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii naamini utakumbuka kuwa hivi karibuni tulianza mada hii kuhusu tatizo la kuota kijinyama sehemu ya haja kubwa yaani  bawasiri.

Sasa leo naomba tuendelee na mada hii kwa kufahamu hizi mbinu za ambazo huweza kusaidiakuepuka kupatwa na tatizo hili.

1. Kwanza ni kuzingatia ulaji wa lishe bora ikiwa ni pamoja na matumizi ya mboga za majani, matunda pamoja na kutumia nafaka zisizokobolewa halikadhalika na vyakula vyenye nyuzinyuzi za kutosha.

2. Kujitahidi kunywa maji ya kutosha angalau glasi 6 kwa siku nzima

3. Epuka kukaa na haja kubwa kwa muda mrefu, jitahidi pale unapohisi haja kubwa nenda kamalize haja hiyo haraka iwezekanavyo.

4. Epuka kukaa muda mrefu sehemu moja, unaweza kukaa baada ya muda kisha ukainuka na kutembea tembea kidogo kisha ukakaa tena.

5. Jitahidi kufanya mazoezi ya viungo nayo huwa na nafasi nzuri ya kukuepusha na tatizo hili.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment