Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 September 2016

Hizi ndi aina 4 za juisi za matunda na faida zake kiafya

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com karibu tena tufahamishane mengine kuhusu afya zetu na vyakula kw ujumla.

Leo mdau wangu nimeona nikwambie kuhusu aina mbalimbali za juisi ambazo huwa na faida ndani ya miili yetu.

Juisi ya Machungwa.
Aina hii ya juisi mbali na kuwa na ladha nzuri lakini pia ina faida ndani ya mwili kwani ina kirutubisho kiitwachio antioxidants.

Pia ndani ya juisi ya chungwa kuna vitamin C nyingi ambayo ni nzuri kwa afya ya ngozi,ukuaji wa mifupa pamoja na kuboresha mzunguko wa damu vizuri ndani ya mwili.

Juisi ya Nyanya
Juisi hii nayo inaumuhimimu wake ndani ya miili yetu kwani ina vitamin E ambayo ni nzuri pia kwa afya ya ngozi, lakini pia juisi hii ni nzuri sana kwa shinikizo la chini la damu lakini pia husaidia kuimarisha kinga za mwili.

Juisi ya Karoti.
Karoti ni mojawapo ya juisi bora kwa afya kutokana na kuwa na vitamin A nyingi sana pamoja na vitamin B na madini kama vile 'calcium' iron, magnesium, sodium. Hivyo virutubisho vyote ni muhimu sana kwa mwili.

Juisi ya Apple
Apple ni mojawapo ya tunda ambalo ni zuri hivyo hata juisi yake pia ni nzuri kwa afya. Juisi ya tunda hii ni nzuri kwa afya ya moyo.

Unapokunywa glasi moja ya juisi ya apple kila siku inamaana unakuwa unaimarisha afya ya moyo wako kwani husaidia kupunguza kiwango cha 'cholesterol' kwenye mishipa ya damu, lakini pia apple lina kiasi kingi cha nyuzinyuzi pamoja na vitamin C.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.


No comments:

Post a Comment