Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 8 September 2016

Hizi ndio aina za mazoezi yanayoweza kutoa ahueni kwa wenye shinikizo la damu

SHINIKIZO la damu au presha ambalo kitaalamu huitwa Hypertension au High Blood Pressure ni neno la kitiba linalotumika kueleza hali ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Shinikizo la damu ni muhimu kwa ajili ya kusukuma damu katika sehemu zote za mwili, lakini shinikizo la damu la juu huweza kuleta matatizo na madhara makubwa kiafya.

Shinikizo la damu kwa kawaida husababishwa na kuongezeka msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu, hali ambayo huufanya moyo ufanye kazi zaidi kuliko kawaida ili kuzungusha damu mwilini.

Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupaswa kupanda na kushuka kila siku, kwa baadhi ya watu hubakia juu na hapo ndipo huambiwa kuwa wana shinikizo la juu la damu. Ugonjwa huu kwa kawaida huitwa muuaji wa kimya kimya kwasababu mtu anaweza kuwa nao kwa kipindi kirefu pasipo mhusika kufahamu.

Leo hapa napenda tufahamishane baadhi ya mazoezi ambayo huweza kumsaidia mtu mwenye ugonjwa huu.

Kwanza kabisa ni mazoezi ya kutembea ambayo huweza kufanywa kila siku mara moja au mbili kwa mhusika kutembea taratibu, lakini si kwa umbali mrefu sana.

Pili ni zoezi la kuendesha baiskeli, mgonjwa wa tatizo hili anaweza kuendesha baiskeli jioni kwa mwendo wa kawaida na si umbali mrefu sana jambo ambalo huweza kuwa msaada kwa wenye tatizo hilo.

Kukimbia pia huweza kumsaidia mgonjwa wa tatizo hili licha ya kwamba haipaswi kukimbia kwa mwendo wa haraka na si kwa umbali mrefu.

Mazoezi mengine ni vizuri kupata ushauri  kutoka kwa wataalam wa afya kabla ya kuamua kuanza kuyafanya ili kuepuka madhara zaidi yanayoweza kujitokeza.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment