Sunday, 25 September 2016

Hizi ndio baadhi ya sababu za maumivu ya chini ya kitovu kwa wanawake

Wanawake wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu tatizo la kupatwa na maumivu makali chini ya kitovu na wamekuwa wakipenda kujua maumivu hayo huashiria tatizo gani?

Hivyo leo nimeona ni vyema nikupatia maelezo kuhusu maumivu hayo huashiria tatizo gani hasa.

Kwanza ni kutokukomaa kwa mayai ya uzazi, hali hiyo husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba na hivyo kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu.

Aidha, masuala ya magonjwa ambukizi hususani ya kwenye mfumo wa mkojo (U.T.I) pamoja na kuwa na matatizo ya kibofu cha mkojo hali hizo zote mbili huweza kupelekea maumivu chini ya kitovu.

Pamoja na hayo, pia wale wanawake ambao huwa hawana mpangilio maalum katika mfumo wao wa siku za hedhi hawa nao mara nyingi hukubwa na maumivu haya ya chini ya kitovu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment