Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 11 September 2016

Huu hapa uwezo wa kiazi mviringo katika kuondoa weusi chini ya macho na kulainisha mikono

Viazi mviringo ni moja ya mahitaji ambayo ni rahisi kuyapata sehemu yoyote na wengi wamekuwa wakitumia viazi hivi kutengenezea chips chakula kinachopendwa na vijana wengi hasa wakike.

Pamoja na umaarufu wa viazi hivi mviringo, lakini bado watu hawafahamu viazi hivi kuwa mbali na kutumika katika kutengenezwa kama vyakula huweza kusaidia kuondoa baadhi ya matatizo hasa ya ngozi miilini mwetu.

Mongoni mwa matatizo hayo ya ngozi ni pamoja na kuondoa hali ya weusi chini ya macho ambayo imekuwa ikiwakabili baadhi ya watu na kujikuta wakionekana kutovutia. Hivyo unapotumia kiazi mviringo huweza kutatua tatizo hilo.

1. Kuondoa weusi chini ya macho
Jambo la kufanya ni kukata kipande kidogo cha kiasi kisha tumia kwa kusugua taratibu sehemu yenye hali ya weusi angalau kwa dakika 10. Fanya hivyo kwa siku 10 hadi 15 ili kupata matokeo mazuri zaidi.

2. Pia kiazi hulainisha ngozi ya mikono


Aidha, viazi hivyo pia huweza kusaidia kulainisha ngozi ya mikono, unachopaswa kufanya ni kuchemsha viazi vyako kisha viponde ili kupata rojo yake na baadaye tumia rojo hilo kupaka mikononi mwako kwa kusugua taratibu na kisha kaa nayo kwa muda wa dakika10 ili kupata matokeo mazuri zaidi. Fanya zoezi hili mara kwa mara ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment