Thursday, 22 September 2016

Majani ya ukwaju na uwezo wake wa kutoa ahueni kwa wenye kikohozi


Mara kadhaa tumekuwa tukizungumzia kuhusu faida za juisi ya ukwaju sasa leo naomba tuangazie majani ya ukwaju ambayo huweza kumsaidia mtu ambaye anasumbuliwa na kikohozi kwa muda mrefu.

Tafuta majani ya ukwaju kiasi cha fungu moja la mboga za majani, kisha yatwange halafu weka maji robo lita katika majani hayo yaliyotwangwa na kisha koroga vizuri.

Ukishapata mchanganyiko huo, utahitajika kutafuta asali kwenye ujazo wa kikombe kidogo cha chai kisha changanya na ule mchanganyiko wa majani ya ukwaju uliyoyasaga hapo awali kisha changanya vizuri na asali hiyo na uanze kwa kutumia kwa kunywa asubuhi na jioni kiasi cha kijiko kikubwa cha chakula. Unaweza kutumia tiba hii kwa muda wa wiki moja mfululizo.


Zingatia
Ukihitaji kutumia tiba hii ni vyema uhakikishe kwanza umeshawahi kupima kifua kikuu na ukagundulika huna tatizo, kwani kikohozi cha muda mrefu ni moja ya dalili za kifua kikuu, hivyo kama ni kifuu kikuu ni vyema ukafuata ushauri wa daktari kwani majani hayo huweza kutoa ahueni kwa wale wenye kikohozi cha kawaida tu na si tiba ya kifua kikuu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment