Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 27 September 2016

Mambo matatu muhimu ya kuyajua kuhusu chungwa na faida zakeLeo napenda ufahamu kuwa endapo utapata nafasi ya kula angalau chungwa moja tu kila siku basi tambua wazi kuwa kuna hizi faida hapa chini utakuwa unazzipata kila unapotumia tunda hilo.

Kwanza utauhakikishia mwili wako usalama mkubwa zaidi wa kiafya kutokana na tunda hilo kuwa na kiwango cha kutosha cha vitamin C ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kumfanya mhusiaka kutosongwa na magonjwa ya mara kwa mara kirahisi.

Chungwa lililokatwa vipande viwili

Lakini pia ulaji wa chungwa mara kwa mara utaupatia mwili wako madini ya potassium, calcium, folate,    pamoja na vitamin B ambavyo vyote kwa pamoja ni muhimu ndani ya miili yetu wanadamu.

Pamoja na hayo, chungwa pia lina nyuzinyuzi 'fiber' ambazo huhitajika sana katika kufanya zoezi la umeng'enyaji chakula ndani ya tumbo na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa choo.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment