Monday, 26 September 2016

Mambo usiyopaswa kufanya mara baada ya kula 6


Ni jambo la msingi sana kufuata utaratibu mzuri wa ulaji wa vyakula kwa lengo kuwa na afya bora zaidi,

Kwa kawaida mlo wa usiku ni moja ya mlo muhimu zaidi kwani mara nyingi baada ya mlo huo wengi wetu huwa tunaelekea kulala jambo ambalo husababisha mwili nao kutumia vizuri virutubisho vyote vilivyoingia kupitia chakula.

Leo ninayo haya mambo muhimu ya kuzingatia kabla na baada ya kupata mlo wako wa usiku>>
Epuka kuoga
Kuoga mara baada ya kula huweza kuingiliana na mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni. unapooga mara baada ya kula husababisha kupungua kwa hali joto mwilini.


Kunywa maji ya uvuguvugu.
Kunywa glasi moja ya maji ya uvuguvugu dakika thelathini kabla ya kupata mlo wa usiku, hii itakusaidia sana kurekebisha mfumo wako wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Pia inashauriwa mara baada ya kula usinywe maji hadi ipite angalau nusu saa ndio utaweza kunywa maji yako ya kunywa, hii husaidia mwili kuvyonza virutubisho vizuri mara vinapokuwa vimeingia mwilini tayari kupitia chakula ulichokula.

Kwa kawaida inashauriwa kusubiri dakika 30 hadi 45 mara baada ya kula ndio uoge, lakini ukiona utaratibu huo unakushinda basi unaweza kuoga kwanza kabla ya kwenda kula.

Usilale haraka
Kwa kawaida wengi wetu huwa tuna utaratibu wa kulala mara tu baada ya kula, hali hupelekea kuathiri umeng'enyaji wa chakula hivyo ni vyema kuepuka kulala mara baada ya kula na badala yake inatakiwa usubiri angalau saa 2 zipite ndio uweze kupanda kitandani kulala.

Unachopaswa kufanya mara baada ya kula unaweza ukafanya maandalizi ya kazi zako za kesho au kuzungumza na familia ili tu kuepuka kupanda kitandani mara baada ya kula.

Epuka kufanya mazoezi mazito
Mara baada ya kula usiku jitahidi uepuke kufanya shughuli za kutumia nguvu sana kwani kumbuka wakati huo mwili unakuwa upo katika harakati za umeng'enyaji wa chakula na endapo ikatokea utafanya shughuli nzito mara baada ya kula usiku basi huenda ukakumbwa na maumivu ya tumbo pia.

Kusafisha meno.
Unapomaliza kula na kabla ya kuelekea kulala hakikisha unasafishwa kinywa chako kwa kupiga mswaki, lakini zingatia kwamba unapaswa kupiga mswaki mara baada ya dakika thelathini.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.


No comments:

Post a Comment