Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 21 September 2016

Matumizi ya maua ya Mlonge kiafya


Maua ya mti wa mlonge yana msaada mkubwa katika matibabu na miongoni mwa faida kubwa ya maua ni kumsaidia mama anayenyonyesha kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa.

Sanjari na hayo, maua ya mlonge pia husaidia kutibu matatizo ya mkojo kutoka kwa shida au mkojo kutoka huku ukiambatana na maumivu makali, hivyo basi matumizi ya maua ya mlonge huweza kuondosha matatizo hayo.

Maandalizi ya maua ya mlonge 
Inabidi yachemshwe na kupata mfano wa chai iliyotokana na maua ya mlonge ambayo mhusika atahitajika kunywa chai hiyo kila siku kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Kimsingi mti wa mlonge una faida nyingi sana na ni ngumu kuzimaliza zote kwa mara moja, lakini kwa leo naomba tuishie hapo lakini kama utakuwa na maswali unaweza kuwasiliana nami kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment