Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 13 September 2016

Njia 3 za asili ambazo huweza kukausha vidonda haraka


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele leo, lakini kama utakuwa haupo vizuri labda unaumwa basi tovuti hii pia inaweza kukusaidia kukupa njia za kumaliza tatizo lako kupitia ushauri wetu pia. Karibu sana

Moja ya mambo ambayo napenda kuzungumzia kwa sasa ni kukufahamisha mambo ya kufanya pale unapopatwa na jeraha au kidonda.

Huenda labda ukawa nyumbani unafanya shughuli zako na bahati mbaya ukajikata na kisu na kusababisha jeraha au chochote kile kikakufanya kupatwa na jeraha basi usipate shida fanya haya yafuatayo:

Kwanza tambua kwamba unapopatwa na jeraha huweza kuwa moja ya njia ya kusababisha kupatwa na maambukizi mengine kupitia jeraha hilo hivyo ni vyema ukazingatia haya yafuatayo kila unapopatwa na jeraha.

Asali

Asali ni moja ya suluhisho nzuri pale unapopatwa na jeraha unachopaswa kufanya paka kiasi cha asali kwenye jeraha hii itasaidia kukuepusha kupatwa hata na maambukizi mengine kupitia jeraha lako.

Aloe Vera
Pia unaweza kutumia aloe vera unachotakiwa kufanya ni kutafuta tawi la mmea wa aloe vera kisha likate na mara baada ya kukata utapata ule utomvu wake kisha utapaka sehemu uliyopatwa na jeraha lako na itakusaidia kupata uponyaji. rudia kufanya hivyo kila baada ya muda.

Ukwaju.
Ukwaju ni njia nyingine ya kukabiliana na majeraha madogo madogo (vidonda) na huu ukwaju huweza kusaidia kuzuia utokaji wa damu zaidi kwenye jeraha.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment