Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Friday, 9 September 2016

Njia 3 za asili ambazo zitakusaidai kuondoa weusi kwenye kwapa haraka


Baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na weusi sehemu za makwapa, hali ambayo huwakwaza hasa zaidia kinadada na kujikuta wakishindwa kuvaa baadhi ya mavazi kwa kuhofia hali hiyo.

Leo ninazo hizi mbinu za asili za kupunguza au kuondoa tatizo hilo

Mafuta ya nazi na ndimu
Mafuta ya nazi hutumika kulainisha ngozi lakini yanapochanganywa na ndimu huweza kuondoa weusi wa sehemu za kwapa.

Unachopaswa kufanya ni kuchukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi kisha changanya na ndimu kijiko kimoja na upake sehemu yenye tatizo huku ukisugua taratibu, kisha kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kisha nawa fanya hivyo kwa wiki 2 utaona mabadiliko.

Ndimu, sukari, asali.
Unaweza pia kutumia mchanganyiko huu na ukaona pia mafanikio kwa tatizo hilo. Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu kijiko pamoja na kijiko kimoja cha sukari.

Baada ya hapo paka mchanganyiko huo sehemu yenye tatizo kwa kusugua taratibu na uache mchanganyiko huo kwa mda wa dakika 10 hadi 15 kabla ya kunawa.

Ganda la chungwa na asali
Kamua maji ya ganda la chungwa kwenye kikombe kisha changanya na asali kijiko kimoja kidogo kisha paka mchanganyiko huo sehemu iliyoathirika. Fanya zoezi hili kwa wiki mbili ili kupata matokeo mazuri.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment