Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 7 September 2016

Tumia njia hizi 2 ili kupunguza tatizo la maumivu ya matiti

Baadhi ya wanawake wamekuwa wakilalamika kutokana na kuhisi maumivu kwenye matiti na kushindwa kujua nini cha kufanya.

Kwanza napenda ifahamike kuwa maumivu haya ya matiti huweza kutokea kwenye matiti yenyewe au pembeni yake (karibu na kwapa.) na kitaalamu tatizo hili hufahamika kama 'mastalgia'.

Mwanamke mwenye tatizo hili huweza kuhisi maumivu pale unapoyashika matiti, jambo ambalo hupelekea wanawake kupata hofu zaidi, huku wengine wakihisi kuwa ni dalili ya saratani.

Aidha, maumivu hayo yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote, huku yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda.

Kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha maumivu ya matiti kama hizi zifuatazo:

Kukoma kwa hedhi (menopause)
Hali ya mabadiliko ya vichocheo vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. hali hiyo huchangia matiti kujaa na kuuma na kusababisha mumivu hayo.
Maambukizi ya matiti
Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
Kutanuka kwa mirija ya maziwa
Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.

Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kwamba mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani, lakini zifuatazo ni njia ambazo huweza kukupati ahueni ikiwa unatatizo hilo:

1. Kuvaa sidiria isiyokubana
2. Punguza unywaji wa chai na kahawa

Ikiwa unaona hali inaendelea ni vyema kuonana na wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment