Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 1 October 2016

faida 4 muhimu za juisi ya broccoli na sehemu ya kuipata ikiwa tayari imeshaandaliwaBroccoli ni aina ya mbogamboga ambayo inataka kufanana sana na kabeji, lakini yenyewe majani yake huwa na muonekano wa kijani sana tofauti na ilivyo kwenye kabeji.

Mara nyingi mbogamboga hii hutumiwa sana na wahindi na hata kupatikana imekuwa ikipatikana sana kwenye masoko yanayotembelewa sana na watu wa jamii hiyo.

Mbogamboga hizi zinapoandaliwa vizuri na kupata juisi yake huwa na manufaa zaidi na miongoni mwa faida za mbogamboga hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:

Husaidia kuzalisha chembe nyekundu za damu
Broccoli imekuwa na kiwango kizuri cha madini ya chuma ambayo husaidia kuzalisha chembe nyekundu za damu ndani ya mwili na hivyo huweza kumsaidia mtumiaji wa juisi hii kuepuka tatizo la upungufu wa damu.

Husaidi kukinga dhidi ya saratani
Kutokana na kuwa na vitamin B2 na mirutubisho cha  'riboflavin' na 'antioxidant' ambayo husaidia kuulinda mwili dhidi ya seli ambazo huweza kusababisha saratani za aina mbalimbali.

Husaidia kulinda afya ya mifupa na meno
Ndani ya juisi ya broccoli kuna madiniya calcium ambayo husaidia kulinda afya ya mifupa, lakini pia husaidia kupunguza maumivu ya viungo mwilini.

Juisi ya broccoli iliyoandaliwa
Ni nzuri kwa afya ya macho
Juisi hii husaidia kuboresha afya ya macho hususani kwa wale wenye uoni hafifu nyakati za usiku, lakini pia juisi hii husaidia macho kutopata madhara mbalimbali yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Kama unahitaji juisi hii ya broccoli unaweza kufika Mandai Natural Food iliyopo Ukonga Mongolandege jijini Dar  es Salaam, utaipata ikiwa tayari imeshaandaliwa vizuri kabisa. Au tupigie simu kwa msaada zaidi kuhusu namna ya kuiandaa namba zetu ni 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com 

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment