Monday, 17 October 2016

Faida 2 muhimu utakazopata kwa kutumia majani ya mgomba


Mgomba ni mmea ambao huzaa matunda yaitwayo ndizi ambayo ni matunda ambayo hupendwa na watu wengi zaidi.

Mara kadhaa tumeshazungumza kupitia tovuti hii kuhusu umuhimu wa ndizi na faida zake kiafya, lakini leo nimeona tufahamishane kuhusu faida za majani ya mgomba yenyewe ni kwa namna gani yanaweza kutumika kwa manufaa.

Majani haya yakitumika vizuri huweza kusaidia kutuliza maumivu ya kichwa ambayo hujitokeza kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchovu wa shughuli mbalimbali na mihangaiko ya kila siku.

Aidha, majani hayo yakipondwa na kuwekwa kwenye vidonda vibichi husaidia kidonda kukauka kwa haraka na kupona.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment