Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 4 October 2016

Faida 5 muhimu za kunywa juisi ya miwa kila siku


Miwa ni moja ya zao muhimu ambalo hutumika katika kukamilisha uzalishaji wa sukari. Hata hivyo zipo faida kadhaa za matumizi ya juisi ya miwa kiafya.

Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili, lakini pia matumizi ya juisi hii husaidia kuongeza baadhi ya virutubisho mwilini.
Miwa ambayo ipo tayari kutengenezwa juisi
Virutubisho hivyo ni pamoja na madiniya chuma, magnesium, calcium ambayo yote ni muhimu nadni ya mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya ya mifupa pamoja na damu.

Aidha, juisi hii pia husaidia kwa wale wenye shida ya matatizo ya mkojo 'urinary tract infections', pamoja na kulinda afya ya figo.

Matumizi ya juisi ya miwa pia husaidia kuboresha umeng'enyaji wa chakula ndani ya tumbo na hivyo kupunguza uwezekano wa ukosefu wa choo.

Pamoja na hayo, juisi hii inamadini ambayo husaidia kulinda afya ya meno.

Kama utahitaji maelekezo zaidi kutoka kwetu basi usipate shida unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment