Monday, 3 October 2016

Faida 5 za juisi ya kiazi kikuu na sehemu pakuipata


Kiazi kikuu ni aina ya kiazi ambacho muonekano wake hufanana na kitunguu kiasi, lakini chenyewe huwa na rangi nyekundu zaidi.

Kiazi hiki mara nyingi hupatikana kwenye masoko mbalimbali hapa nchini, lakini zaidi huweza kupatikana kwenye masoko ambayo mara nyingi hutembelewa na wageni hususani wenye asili ya kihindi au maarufu kama masoko ya uzunguni.

Hapa leo napenda nikufahamishe faida kadhaa ambazo huweza kupatikana kwa kutumia glass moja ya juisi ya kiazi kikuu kila siku:-

1. Husaidai kupunguza sumu ndani ya mwili
Hii ni kwasababu juisi hii huenda kuisaidia ini na kulifanya kufanya kazi yake ya kuchuja sumu vyema ndani ya mwili.

2. Huimarisha umeng'enyaji wa chakula ndani ya mwili
Juisi hii husaidia kwenda kuamsha uvunjaji wa chakula ndani ya tumbo, hivyo unaweza kupata faidi hii endapo utatumia angalau nusu kikombe tu ya juisi hii kila siku.
10 Reasons To Have A Glass Of Beet Juice Every Day
Glasi moja ya juisi ya kiazi kikuu hutosha kabisa kutoa matokeo mazuri endapo itaandaliwa ipasavyo na kutumika mara kwa mara
3. Huimarisha tendo la ndoa
Tafiti zilizowahi kufanyika zilionesha kuwa ndani ya kiazi kikuu kuna madinu yaitwayo 'boron' ambayo husaidia kuzalisha homoni za kushiriki tendo la ndoa, lakini pia husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini ambayo pia ni sehemu ya manufaa kwenye tendo la ndoa.

4. Huimarisha kinga za mwili.
Juisi ya kiazi kikuu imeshehenni vitamin C, ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili ndani ya mwili.

5. Huboresha afya ya ngozi
Juisi hii husaidia kuondoa seli mfu ndani ya mwili na hivyo kuboresha afya ya ngozi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna sahihi ya kuandaa juisi hii ya kiazi kikuu tupigia simu kwa namba zifuatazo ili tukusaidie: namba zetu ni +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Juisi hii unaweza kuipata Mandai Natural Food iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Kummbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment