Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 28 October 2016

Haya hapa matunda matano yenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume


Habari za leo mdau wangu wa tovuti yetu ya www.dkmandai.com bila shaka utakuwa upo vizuri karibu tuendelee kufahamishana umuhimu wa lishe bora pamoja na matunda mbalimbali kiafya.

Leo ninayo orodha ya matunda ambayo huweza kusaidia kupunguza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na virutubisho yaliyonayo.

1. Embe 

Kwa embe hili linauwezo wa kupunguza tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kuwa na vitamin E ambayo huwa na nafasi kubwa ya kuongoza hisia za kushiriki tendo la ndoa.

2. Tikitimaji


Hili ni miongoni mwa tunda nzuri pia kwa wenye tatizo hilo kwani husaidia kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mwili jambo ambalo huweza kumsaidia mwanaume mwenye upungufu wa nguvu za kiume kupata ahueni.

3. Komamanga

Tunda hili lina kirutubisho kiitwacho antioxidants ambacho nacho huimarisha mzunguko wa damu kuwa vizuri ndani ya mwili na hivyo kupunguza ukubwa wa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

4. Parachichi

Ndani ya tunda hili kuna utajiri wa madini ya potassium, vitamin B6, vitamin E kwa pamoja virutubisho hivyo husaidia kuboresha afya ya moyo na kurekebisha mzunguko wa damu kuwa vizuri zaidi.

5. Ndizi

Ndani ya ndizi kuna madini ya potassium ambayo pia huwa na mchango kwenye masuala ya tendo la ndoa.

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment