Friday, 7 October 2016

Hizi hapa njia rahisi za kupunguza unene


Watu wengi wamekuwa wakipata shida kuhusu suala la uzito kupita kiasi na kushindwa kutambua namna gani sahihi ya kukabiliana na tatizo hili.

Hapa ninazo njia kadhaa zitakazokusaidia kupunguza uzito wa mwili wako:-

Weka mbali vyakula na vinywaji  visivyokuwa vya lazima
Ni vyema kuweka mbali vyakula visivyokuwa vya lazima yaani vile viburudisho kama vile soda  na vingine vingi vyenye asili hiyo.

Kunywa maji mara kwa mara
Jenga utaratibu wa kunywa maji mara kwa mara hasa kabla ya kula zoezi hili huweza kusaidia kupunguza uzito mkubwa wa mwili  endapo zoezi hilo litafanyika mara kwa mara.

Utulivu wakati wa kula
Unapokula hakikisha upo sehemu tulivu na huna shughuli nyingine zaidi ya kula tu, kwani baadhi ya watu hula huku wakiangali runinga au wakichezea simu au kopyuta. hali hii huweza kuchangia mhusika kula zaidi kuliko pale anapokula bila kuwa na shughuli nyingine.

Pata muda wa kutosha wa kulala
Hali ya kukosa usingizi wa kutosha huchangia kuharibu hamu ya chakula, na baadaye kuchangia kuvurugika kwa mpangilio wa mlo wako au ratiba ya kula na hivyo kujikuta ukiingia kwenye tatizo hilo la unene kupita kiasi hivyo ni vyema kupata muda wa kutosha wa kulala kwa faida zaidi.

Punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari
Vinywaji hivyo huchangia kuongezeka kwa tatizo hilo la uzito mkubwa hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vinywaji hivyo ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment