Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 1 October 2016

Hizi hapa sababu za unene uliokithiri & kitambi


Unene ni ile hali ya mtu kuwa na uzito mkubwa kuliko uzito ambao unatakiwa  kiafya kuingana na mhusika.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia unene kupita kiasi kwa watu:-

Ulaji kupita kiasi
Ulaji wa kupita kiasi huweza kuchangia tatizo hili, na mara nyingi huweza kuonekana endapo mhusika anajitahidi kula kwa bidii lakini hana shughuli zinazomfanya kukitumia chakula hicho ipasavyo ndani ya mwili.Hali hiyo huchangia mwili kubaki na mafuta mengi na kukosa kwa kuayapeleka na matokeo yake mhusika huanza kujikuta anapata kitambi.

Kutofanya mazoezi
Mazoezi ni muhimu sana katika kuuweka mwili wako katika hali ya kiafya na mazoezi hayo ni vyema yakawa yakudumu na yakawa sehemu ya maisha yako. Jitahidi angalau kwa siku upate hata nusu saa tu ya kufanya maziwa.

Kushindwa kula kiafya
Wengi wetu tunakula bila kuzingatia taratibu za kiafya na kujikuta tukiingia kwenye tatizo hilo, hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa lishe na kupata ushauri wa namna bora ya kula kiafya.

Matumizi ya dawa
Kuna baadhi ya dawa huweza kuchangia tatizo hili hususani mhusika hatajihusisha kabisa na mazoezi, hivyo ni vyema kuzingatia hilo, lakini kupata ushauri kwa wataalam kabla ya matumizi ya dawa.

Hayo ni machache, lakini kwa mengine mengi zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.No comments:

Post a Comment