Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 28 October 2016

Hizi ndio dalili za upungufu wa nguvu za kiume

Habari msomaji wa www.dkmandai.com kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri basi utakuwa unafahamu kuwa tayari tulianza kuzungumzia tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume na tulizungumzia sana kuhusu sababu za tatizo, leo tuangazie dalili zake pia. Karibu

Dalili za tatizo hili si rahisi kuonekana endapo mtu atakuwa hashiriki tendo hilo. Hii ni kwasababu suala la nguvu za kiume ni ukamilifu wa tendo, lakini wengi hufanikiwa kushiriki tendo shida inakuja kwenye kulikamilisha tendo au kushindwa kusimamisha.

Mbaya zaidi wanaume wengi wamekuwa wakijitathimini ubora wao katika tendo kulingana na saa wanazoweza kufanya tendo hilo, lakini hiyo si njia sahihi ya kipimo cha uwezo wa kushiriki tendo hilo.

Kimsingi muda si kipimo cha nguvu za kiume, nguvu ni ule uwezo wa kukamilisha lile tendo kuanzia mwanzo hadi mwisho, unaweza ukawa umechukua sekunde mbili, lakini kama umelifanya na likakupa matokeo yale yanayostahili basi hilo tendo ni kamilifu halina mapungufu yoyote

Pamoja na hayo, suala hili pia hutegemea sana namna ulivyojiandaa kisaikolojia katika siku ya tendo hilo.

Kwa mfano siku umechoka sana na unapokosa hamu ya tendo la ndoa basi tegemea kuchukua muda mrefu zaidi kumaliza, lakini siku ambayo utakuwa umejiandaa kisaikolojia itakuchukua muda mfupi kumaliza tendo, kwa sababu kuna uhusiano mkubwa kati ya tendo na fikra za mtu.

Udhaifu wa tatizo hili huweza kubainika endapo mhusika atakuwa akishindwa kufanya tendo hilo kwa kila mwanamke na endapo hali hiyo itakuwa ikijirudia mara kwa mara.

Hata hivyo, ni vizuri jamii hususan vijana wakafahamu tatizo hili huchangiwa na maandalizi hafifu ya tendo hilo. Hivyo kitu muhimu ni maandalizi ya kutosha.

Pamoja na hayo, imefika wakati sasa wa kujenga tabia ya kupanga ratiba ya matendo ya ndoa na siyo kukurupuka tu, lakini pia kuna umuhimu mkubwa wa kutibu magonjwa yote bila kujali ni ya ngono au la! Jambo ambalo husaida kupunguza tatizo hilo.

Pia tatizo hilo huweza kudhibitiwa kwa kula vyakula asilia hususani vya nyuzinyuzi ambavyo vimesheheni nishati nyingi.

Vyakula vya nafaka husaidia kuzalisha homoni za ‘testosterone’ kwenye damu pamoja na kumuwezesha mhusika kuwa na nguvu na hatimaye kuongeza kiwango cha uwezo wa kushiriki tendo.

Ulaji wa nafaka zisizokobolewa hufaa zaidi kiafya kuliko zile zinazokobolewa kwani husaidia kuupa mwili nguvu zaidi na hivyo kusaidia kuongeza uwezo wa nguvu za kiume.

Tangawizi nayo ni kiungo kizuri na muhimu katika kuongeza nguvu za kiume, kwani husaidia kusisimua mfumo wa mzunguko wa damu mwilini.

Damu inapozunguka vizuri mwilini huwezesha kufika kirahisi sehemu za viungo vya uzazi ikiwa ni pamoja na uume.

Vyakula vingine ambavyo ni muhimu katika kuimarisha tendo la ndoa na kuongeza nguvu za kiume ni pamoja na karanga, ambazo zina kiwango cha madini ‘magnesium’ na zinki ambayo yana umuhimu mkubwa katika uzalishaji wa mbegu za kiume.

Mbali na vyakula hivyo, asali nayo hufaa kwa mtu mwenye shida ya upungufu wa nguvu za kiumea ambaye anaweza kuamua kila siku asubuhi na jioni akawa anapata angalau kijiko kimoja cha chakula cha asali.

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:-  0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment