Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 27 October 2016

Je, unafahamu huu uwezo mwingine wa chungwa kiafya?


Kuzingatia lishe bora ni moja ya mambo muhimu kwa afya zetu wanadamu na kuna baadhi ya madhara ambayo huweza kujitokeza kwa kutozingatia ulaji wa lishe bora.

Ulaji mbovu wa vyakula visivyo na lishe bora ni miongoni mwa sababu ambazo huweza kuchangia matatizo mbalimbali kiafya ikiwa ni pamoja na kufunga choo.

Zifuatazo ni miongoni mwa sababu ambazo hupeleka kufunga choo:-

1. Ulaji wa vyakula vilivyokobolewa.
2. Kutokunywa maji ya kutosha
3. Kula vyakula bila mpangilio mzuri
4. Matumizi holela ya baadhi ya dawa
5. Kukosa mazoezi ya kutosha

Ili kumaliza tatizo la kukosa choo unaweza kufanya yafutayo:-

Machungwa
Kula machungwa angalau mawili asubuhi kabla ya kula chochote, hivyo hivyo pia utakula machungwa mawili kabla ya kulala. Unaweza fanya hivyo angalau ndani ya wiki moja.

Machungwa yanauwezo wa kusaidia tatizo hilo kutokana na kuwa na 'roughage' ndani yake.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment