Sunday, 2 October 2016

Je, unaijua juisi ya kiazi kitamu? Zipo hapa faida zake 5 kiafya

Najua si rahisi sana kuamini kwamba kiazi kitamu kinaweza kutumika kuandaa juisi na ukapata kinywaji kizuri tu ambacho kitakuwa kimeambatana na manufaa kadhaa kiafya.

Saa leo napenda ufahamu kuwa kiazi kitamu huweza kutengenezwa na kuwa kimiminika yaani juisi ambayo inapotumiwa huwa na faida zifuatazo:-

Miongoni mwa faida ya juisi ya viazi vitamu ni pamoja na kusaidia kuimarisha kinga za mwili, afya ya mifupa pamoja na kuboresha afya ya ngozi.

Aidha, juisi hiyo pia husaidia kupunguza hatari ya mtumiaji kupatwa na aina mbalimbali za saratani kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants' .

Pamoja na hayo, juisi hii pia huwa na nafasi ya kutoa ahueni kwa wale wenye kisukari kwani husaidia kurekebisha sukari ndani ya mwili.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna sahihi ya kuandaa juisi hii ya viazi vitamu usisite kutupigia simu kwa namba zifuatazo ili tukusaidie: namba zetu ni 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment