Wednesday, 5 October 2016

Juisi ya pera na faida zake zipo hapa

MTI wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda inayofahamika na wengi hapa nchini. Mti huu hutoa matunda yanayofahamika kama mapera.

Leo tutafahamishana zaidi kuhusu juisi ya matunda haya (mapera) ili kufahamu faida zake kiafya.

Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C, hivyo huwa na nafasi kubwa ya kuimarisha kinga ya mwili kwetu sisi binadamu.

Aidha, mapera pia yamesheheni vitamin A, ambayo husaidia kuboresha afya ya macho na kuwa na uoni mzuri zaidi.

Juisi ya pera inaelezwa kuwa msaada kwa wale wenye tatizo la kisukari kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari na kiwango kikubwa cha 'fiber' ambayo husaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Kama utahitaji maelekezo zaidi kutoka kwetu basi usipate shida unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment