Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 4 October 2016

Mbinu za kutunza fedha na faida zake
Moja ya mambo ambayo tunatamani kuona katika jamii ni mafanikio kwa watu wengine na kuondokana na hali ya umasikini.

Zifuatazo ni mbinu ambazo huweza kukusaidia kuhifadhi fedha na kujikuta unafanikiwa:-

Kupunguza matumizi yasiyo yalazima.
Punguza manunuzi ya vitu vyenye gharama kama vile urembo, nguo, viatu kwani huweza kukusaidia kupunguza matumizi na kiasi kinachobaki ukahifadhi kwa ajili ya baadaye.

Tenga mahitaji ya muhimu
Jitahidi kutenga mahitaji yote ya muhimu na kuepuka manunuzi ya bidhaa za vitu visivyo vya lazima. Andaa orodha ya vitu unavyopaswa kununua kila unapotaka kufanya manunuzi yoyote. Acha tabia ya kununua kila unachokiona

Kaa mbali na starehe 
Hii itakusaidia kufikia malengo yako na kujikuta ukiepuka matumizi mabaya ya pesa na kuwa rahisi kwako kutimiza malengo yako ya baadaye. Ukifanya hivi lazima utapata fedha kiasi ya kuhifadhi ambayo baadaye inaweza kukusaidia kufanya kitu kikubwa zaidi.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment