Friday, 7 October 2016

Njia sahihi ya kutunza mikono yako ili kuepuka magonjwa

Mikono ni miongoni kati ya kiungo ambacho binadamu hukitumia sana katika kazi mbalimbali za kila siku.

Mingoni mwa majukumu ya mikono ni pamoja na kusalimiana na watu, kushika vitu, kutokana na majukumu hayo na mengine kadhaa utabaini kuwa mikono ipo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya magonjwa.

Sasa mambo yafuatayo yanafaa kuzingatiwa ili kuboresha mikono yako:-

Kunawa mara kwa mara
Jitahidi kunawa na sabauni kila wakati kabla ya kufanya chochote, mfano ukitoka chooni, kabla ya kula, ukimaliza kufanya usafi, ukirudi nyumbani kabla ya chochote ni vyama ukanawa mikono. Zoezi hili litasaidia kuweka mikono yako safi na kuzuia kusambaa kwa vijidudu vinavyoweza kuwa chanzo cha  magonjwa. 

Matunzo ya vidole vya mikono
Epuka kucha zako kutunza uchafu kwa ndani, hivyo ni vyema kukata kucha kila mara zinapokua ili kurahisisha namna ya kuzisafisha.

Kumbuka kuwa si vyema kumshika mtoto mchanga kabla ya kunawa mikono, watoto wadogo wako katika hatari ya kuambukizwa haraka na magonjwa.

Pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment