Saturday, 8 October 2016

Tazama video ya Rais wa NGO'S akizima moto uliokuwa ukiteketeza nyumba

The Work Up Tanzania (WUTA) ni NGO'S ambayo hujihusisha na utoaji wa huduma mbalimbali katika jamii.

Shirika hili ambalo makao makuu yake ni Ukonga, eneo la Mongolandege limekuwa likijihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii jijini Dar es Salaam.

 Shirika hili linamalengo makuu matatu ambayo ni kupambana na umasikini, magonjwa amoja na ujinga, ambayo yote hayo shirika limelenga kupambana nayo hasa kwa kutumia rasilimali zinazolizunguka shirika na maisha yetu ya kila siku.

Kwa kuwa shirika linamalengo ya kupambana na umasikini katika jamii kwa namna mbalimbali hapa kuna video ambayo inamuonesha rais wa shirika hilo akisaidia kuzima moto uliokuwa ukitekeza nyumba iliyopo eneo la Mongolandege siku ya Octoba 06/2016 ikiwa ni sehemu ya kuinusuru jamii kuzidi kudidimia kwenye dimbwi la umasikini kutokana na mali zao kuteketea kwa moto.

Unaweza kuitazama video hiyo hapo chini ikiomuonesha Rais wa The Work Up Tanzania akitoa msaada wake kuzima moto huo:-Kwa msaada zaidi au ushauri wa mambo mablimbali yakiwemo ya kiafya unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment