Monday, 3 October 2016

Zifahamu faida za juisi ya boga na sehemu ya kuipata

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com imani yangu kwamba unaendelea vizuri popote pale ulipo unaposoma makala hizi fupi.

Tayari tumewahi zungumza mara kadhaa kuhusu boga, lakini leo napenda tuzungumze kuhusu boga lakini tuangalie faida za juisi yake.

Najua kwa baadhi ya watu itakuwa ni jambo la kushangaza kusikia kuhusu juisi ya boga lakini hakuna kitu ambacho kinashindikana chini ya jua.

Zipo faida kadhaa za matumizi ya boga na hapa napenda kukufikishia hizi baadhi>>>>>>

Juisi ya boga inauwezo mzuri wa kupambana na shinikizo la juu damu pale unapokunywa mara kwa mara hii ni kwa sababu ndani ya boga kuna kirutubisho kiichacho 'pectin' ambayo hufanya kazi kubwa ya kushusha cholesterol na hivyo kupambana na matatizo ya shinikizo la damu.

Huimarisha kinga za mwili, juisi ya boga ina virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini pamoja na vitamin, ambavyo ni muhimu sana kwa kuimarisha kinga za mwili ndani yetu.

Juisi ya maboga haisaidii tu shinikizo la damu na kuimarisha kinga za mwili bali husaidia sana kumkinga mhusika dhidi ya matatizo ya shambulio ya moyo pamoja na kiharusi 'stroke'

Aidha, matumizi ya juisi hii ni muhimu sana kwa afya ya figo na ini katika hili juisi hii itakusaidia zaidi pale unapokunywa mara tatu kwa siku yaani asubuhi mchana na jioni kila siku kwa kufanya hivyo husaidia sana hata kuondosha mawe kwenye figo.

Pamoja na hayo, juisi hii ni nzuri kwa kurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni,'digestion system' kutokana na kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi 'fiber' za kutosha hivyo juisi hii ni kinga tosha ya matatizo kukosa choo mara kwa mara.

Ndugu msomaji wangu hizo ni faida kadhaa za matumizi ya juisi ya boga, napenda kukuahidi kwamba bado ninazo faida nyingine za juisi hii ya boga endelea kutembelea tovuti hii mara kwa mara ili kuayafahamu mengine mengi kuhusu faida hizi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna sahihi ya kuandaa juisi hii ya boga tupigia simu kwa namba zifuatazo ili tukusaidie: namba zetu ni 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Juisi hii unaweza kuipata Mandai Natural Food iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment