Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 November 2016

Chanzo cha maumivu ya mgongo na jinsi ya kukabiliana nayo


Maumivu ya mgongo ni moja ya  tatizo mbalo huweza kumpata mtu yoyote katika maisha yake, lakini pia tatizo hili huweza kuwa ni moja ya vyanzo vya ulemavu endapo mhusika hatapata matibabu ya uhakika.

Utafiti unaonyesha kila mtu hupata maumivu ya mgongo angalau mara moja kwenye kipindi cha maisha yake.

Tatizo hili huweza kuanza ghafla au kwasababu ya kuanguka au kubeba kitu kizito lakini pia huweza kuanza taratibu kutokana na sababu ya magonjwa fulani fulani yanayoshambulia mifupa, nyama au mishipa ya fahamu ya mgongo.

Pia tatizo la maumivu ya mgongo huweza kuchangiwa na kufanya mazoezi holela bila kupata ushauri wa wataalam.

Bahati nzuri zipo njia kadhaa asili ambazo huweza kupunguza maumivu ya mgongo ukiwa nyumbani.

Yafuatayo ni matibabu ambayo hayahusishi dawa na huweza kufanywa na mhusika akiwa nyumbani:-

Kuhakikisha unachunguza na kutambua chanzo cha maumivu yako na ikiwa umetambua chanzo basi ni vyema kukifanyia kazi. Mfano  chanzo ikiwa ni kubeba vitu vyenye uzito mkubwa au kulala na mto kitandani. Unachopaswa kufanya ni kuepuka vyanzo hivyo.

Kufanya mazoezi, haya ni mazoezi ya kitaalamu ambayo hupaswa kushauriwa na wataalam wa afya au kufanyiwa na mtaalamu wa afya ya physiotherapy au mtu yeyote wa afya anayejua jinsi ya kuyafanya. 

Kimsingi mazoezi hayo husaidia kupata nafuu kwani huweza kurudisha kila kiungo kwenye sehemu yake ya zamani hasa matatizo ya pingili za mgongo. 

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.No comments:

Post a Comment