Friday, 11 November 2016

Fahamu faida 4 muhimu za majani ya mlonge

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii bila shaka utakumbuka kuwa nilikuletea faida za mmea wa mti wa mlonge.

Pia tulishazungumza kuhusu faida za mbegu za mlonge na sasa tutakwenda kuangalia faida za majani yake kwa ufupi.

Majani ya mlonge yanapotengenezwa kama juisi hutumika kusafisha tumbo na kutibu magonjwa ya zinaa, lakini pia juisi inapochanganywa na asali husaidia kutibu kuharisha.

Pia juisi hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wale wenye presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.

Majani hayo ya mlonge pia huweza kupakwa mwilini kwa lengo la kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.

Utafiti wa kisayansi umeonesha kuwa majani ya Mlonge ni chanzo kizuri cha virutubishi vingi sana ikiwa ni pamoja na vitamin C, vitamin A, Calcium na Potassium pia.

Kuna mengi yakuyafahamu kuhusu majani haya ya mlonge na faida zake na si rahisi kuyaeleza yote hapa, hivyo kama utapenda kujua zaidi na namna nzuri ya kutumia majani haya piga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment