Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 November 2016

Fahamu faida za kuoga na maji yapi ni sahihi kwa kuoga yamoto au yabaridi?


Kwa kawaida miili yetu huhitaji matunzo ili kuendelea kuwa na afya bora na moja ya mambo ya msingi ni usafi.

Usafi wa mwili unajumuisha kuoga na kuvaa nguo safi. Kuoga ni kitendo cha kueneza maji kwenye mwili kwa namna yoyote ile.

Baadhi ya watu hujiuliza ni mara ngapi mtu huhitaji kuoga kwa siku, lakini swali hilo linaweza kujibiwa kama ifuatavyo ili ujue mtu anapaswa kuoga mara ngapi kwa siku kwanza itategemea na aina ya kazi anayoifanya  mhusika pamoja na hali ya hewa ya eneo alilopo.

Mfano kama kazi yake inasababisha mtu kutokwa jasho sana na anapata muda wa mapumziko ni vyema akaoga halafu baadae akaendelea tena na kazi. 

Kimsingi kuoga kila siku ni kitu cha msingi sana. Kutooga kwa muda mrefu kunaweza kusababisha muwasho na kubadilika kwa rangi ya ngozi.

Ikiwa utashindwa kuoga kila mara kutokana na sababu mbalimbali kama baridi kali sana na uhaba wa maji unapaswa kujisafisha kwa kipande cha nguo kisafi sehemu zote zilizojificha kama kwapani ambapo vimelea hujikusanya kiurahisi na kusababisha madhara au maambukizi.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuogaEpuka kuchangia dodoki hairuhusiwi kwa kuwa ni rahisi kuambukizana magonjwa ya ngozi husani fangasi.

Maji yapi ni sahihi kwa kuoga?
Wataalamu wa afya ya ngozi wanashauri kuoga maji ya uvuguvugu. Maji ya kuoga ya uvuguvugu husaidia kufungua na kutakasa vishimo vya ngozi vilivyo pamoja na vinyweleo.

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

1 comment: