Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 4 November 2016

Fahamu kuhusu umri mzuri wa mwanamke kubeba mimba

Picha kwa msaada wa mtandao
Wataalamu wa afya ya uzazi bado wanaamini kuwa miaka 20 hadi 35 ndio umri sahihi na mzuri zaidi kwa mwanamke kushika mimba na kuzaa, huku wakiamini kuwa matatizo mengi ya uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na huwa zaidi baada ya miaka 40.

Kwa kawaida baada ya mtoto wa kike kupevuka anakuwa na uwezo wa kushika mimba, japokuwa uwezekano huongezeka zaidi kati ya miaka 20-30 na baada ya hapa uwezekano huanza kupungua.

Kwa mujibu wa The American College of Obstricians & Gynecologists uwezo wa mwanamke kuzaa hupungua katika umri wa miaka 32 na hupungua kwa kasi zaidi katika umri wa miaka 37.

Aidha, magonjwa ya njia za uzazi kama Endometriosis na Uterine fibroids huweza kuwatokea zaidi wanawake wenye umri mkubwa na kusababisha mwanamke kutoshika mimba.

Hata hivyo, hii aimaanishi kwamba unapovuka umri huo utashindwa kushika ujauzito hapana hii huweza kutokea kwa wanawake baadhi. Hivyo basi hili lisiwafanye kinadada kukimbilia kuolewa kabla ya kujipanga kwa kuhofia kuvuka umri huo.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba : 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa ushauri huu umeletwa kwako chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment