Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 4 November 2016

Fahamu sababu na dalili za fangasi sehemu za siri


Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa kuwashwa sehemu za siri husababishwa na fangasi tu.

Hivyo kuna haja ya jamii kubadili mtazamo huo kwani si kila muwasho huwa ni fangasi wakati mwingine huweza kuwa ni mzio allergy.

Zipo baadhi ya sababu ambazo huchangia tatizo la muwasho sehemu za siri ambazo ni pamoja na ugonjwa wa upele, maambukizi mengine ya bakteria. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa sehemu hizo nyeti.

Wataalam wa afya wanaeleza kuwa maradhi ya fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia sana jinsia ya kike kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachosababia wao kuathiriwa zaidi.

Hata hivyo, maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiana na mtu mwenye ugonjwa wa fangasi.

Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizo tengenezwa na pamba kwa asilimia 100 kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu, hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.

Dalili za tatizo hili kwa wanaume huonekana pale ambapo kichwa cha uume hubadilika na kuwa chekundu na kuwasha. Ngozi inayozunguka sehemu za siri huwasha, kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.

Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi.

Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza sababisha kutopona kabisa, kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache, pia vimelea vinaweza kujenga usugu wa dawa.

Kumbuka kwamba ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa ushauri huu umeletwa kwako chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment