Friday, 25 November 2016

Hivi hapa viungo vya mapishi ambavyo husaidia kupunguza maumivu


Miongoni mwa matatizo ambayo huwakumbuka watu wengi ni pamoja na hili tatizo la maumivu ya viungo mwilini.

Leo napenda tufahamu hivi viungo ambavyo huweza kusaidia kupunguza tatizo hilo

Tangawizi
Kiungo hiki ni muhimu pia kwa kupunguza maumivu ya viungo mwilini kutokana na kiungo hicho kuwa na uwezo wa kurahisisha mzunguko wa damu kwenda vizuri ndani ya mwili. Hivyo matumizi ya kikombe kimoja cha tangawizi kila siku huweza kuwa msaada kwako ikiwa unatatizo la maumivu ya viungo.

Mdalasini
Kama una maumivu ya viungo pia unaweza kutumia kiungo hiki ambapo unaweza kunywa maziwa yalichanganywa kidogo na mdalasini pamoja na asali kidogo na utaona faida yake.

Binzari
Kiungo hiki kinafahamika sana kwa akina mama na wengine hukifahamu kwa jina la manjano, ili kiungo hiki kiwe msaada kwa tatizo hili utahitajika kupata maziwa kisha changanya na kijiko kidogo cha binzari baada ya hapo chemsha kwa pamoja kisha subiri yapoe kiasi, lakini yasipoe kabisa halafu utatumia pamba kuchua sehemu yenye tatizo.

Pamoja na hayo, kuoga maji ya baridi pia husaidia kupunguza tatizo hili kwani maji hayo husaidia kuamsha misuli ndani ya mwili na kupunguza maumivu ya viungo vya mwili.

Pia na wewe unaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu ya Facebook ukurasa unaitwa Mandai Products Company Ltd au kwenye email ya dkmandaitz@gamail.com kisha utakuwa ukipata majibu yako kupitia website hii, lakini pia unaweza kutupigia kwa simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment