Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 23 November 2016

Hizi ndio sababu 4 za mimba kuharibika mara kwa mara


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele na unaendelea na shughuli zako vizuri kabisa.

Leo nimeona ni vyema tugusie hili suala la kuharibika kwa mimba mara kwa mara angalau tuzifahamu hata sababu zake tu.

Naamini kwamba kila mwanamke anapobeba mimba matarajio yake huwa ni kujifungua salama na baadaye kumfurahia mtoto wake, licha ya kwamba baadhi ya wanawake kwao imekuwa ni ngumu kuifikia hiyo furaha ya kupata mtoto kwani baadhi yao huishia kubeba mimba tu kisha baada ya mda utasikia imetoka!

Leo wacha tuzifahamu sababu ambazo huchangia tatizo hili la kuharibika kwa mimba mara kwa mara kama ifuatavyo>>>
Moja ya sababu ni maambukizi kwenye mji wa uzazi wa mwanamke kuna kitu huitwa Pelvic Inflammatory Diseases (PID) yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi.

Sababu nyingine ambayo huweza kuchangia kuharibika kwa mimba mara kwa mara ni matatizo ya fangasi Candida nazo pia kwa nafasi yake huweza kuchangia tatizo hili.

Historia ya utoaji wa mimba mara kwa mara huweza kuwa sababu ya tatizo hili, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao huweza kuwa katika hatari ya kuingia katika tatizo hili baadaye.

Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}, magonjwa kama kaswende, kisonono,mara nyingi sana huathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kirahisi.

Endapo utakuwa unahistoria ya kusumbuliwa na tatizo hili mara kwa mara unaweza kuwasiliana na wataalam wa masuala ya uzazi kwenye hospitali illiyopo karibu nawe ili kupata msaada zaidi.

Lakini pia kwa maelezo zaidi au ushauri usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

2 comments: