Wednesday, 2 November 2016

Jinsi kitunguu swaumu kinavyoweza kupunguza maumivu ya kiuno


Maumivu ya kiuno ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi mara kwa mara na mara nyingi tatizo hili hujitokeza hasa wanapokuwa katika kipindi  cha hedhi.

Lakini kuna maumivu ya kiuno ambayo huchukuwa muda mrefu bila kutulia au kuwa yanajirudia mara kwa mara kwa muda mrefu.

Kimsingi maumivu haya huweza kuchangiwa na matatizo kwenye kibofu cha mkojo, via vya uzazi au misuli ya nyonga. Kunawakati maumivu hayo huweza kuwa makali kiasi cha kuathiri shughuli zako za kila siku.

Miongoni mwa sababu za maumivu haya ni pamoja na maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya kizazi au mji wa uzazi ambayo husababisha maumivu ya kiuno wakati wote au wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Sababu nyingine ni kuwa na uvimbe vya kizazi ambavyo husababisha maumivu, lakini maumivu yake huwa ya kuja na kuacha. Pia tatizo hili huweza kuchangiwa na mimba kutunga nje ya kizazi.

Pia maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu (Urinary Tract Infection). Huweza kuwa sababu ya maumivu hayo ya kiuno.

Maumivu ya kiuno pia huweza kusababishwa na ajali iliyoleta madhara sehemu za kiuno kwa muhusika au mazingira ya kazi ya mhusika.

Ili kupata matibabu ya tatizo hili la maumivu ya kiuno ni vizuri kwanza kugundua chanzo cha maumivu hayo kwa kufanya utafiti wa kitabibu kisha kufuatiwa na tiba.

Au unaweza kutumia kitunguu swaumu baada ya kukisaga na kutumia rojo yake kupaka sehemu yenye maumivu na kuchua taratibu angalau kwa siku mara mbili ili kupata matokeo mazuri zaidi. Au wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe: dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment