Wednesday, 23 November 2016

Kwanini unapatwa na maumivu chini ya kitovu? Sababu zote zipo hapa


Wanawake wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu tatizo la kupatwa na maumivu makali chini ya kitovu na wamekuwa wakipenda kujua maumivu hayo huashiria tatizo gani?

Hivyo leo nimeona ni vyeama nikupatia maelezo kuhusu maumivu hayo huashiria tatizo gani hasa.

Kwanza kabisa tatizo hili huashiria mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi.

Sababu nyingine ni kutokukomaa kwa mayai ya uzazi, hali hiyo husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba na hivyo kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu.

Aidha, masuala ya magonjwa ambukizi hususani ya kwenye mfumo wa mkojo (U.T.I) pamoja na kuwa na matatizo ya kibofu cha mkojo hali hizo zote mbili huweza kupelekea maumivu chini ya kitovu.

Pamoja na hayo, pia wale wanawake ambao huwa hawana mpangilio maalum katika mfumo wao wa siku za hedhi hawa nao mara nyingi hukubwa na maumivu haya ya chini ya kitovu, lakini hali hiyo yakutokuwa na mpangilio mzuri katika hedhi huchangiwa na tatizo la vifuko vya uzazi kushindwa kukomaza mayai vizuri kwenye vifuko hivyo na hali hiyo huchangia maumivu makali kwa mwanamke husika.

Pia na wewe unaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu ya Facebook ukurasa unaitwa Mandai Products Company Ltd au kwenye email ya dkmandaitz@gamail.com kisha utakuwa ukipata majibu yako kupitia website hii, lakini pia unaweza kutupigia kwa simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment