Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 3 November 2016

Mambo ambayo huchangia U.T.I na namna ya kujikinga


MAAMBUKIZI sugu ya njia ya mkojo  ni maambukizi kwenye njia ya mkojo ambayo hayatibiki kwa urahisi na huweza kuwa yanajirudia mara kwa mara.

Maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kutokea sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo. Ikiwa maambukizi yataathiri kibofu cha mkojo peke yake ni rahisi hali hii kutibika, isipokuwa maambukizi yakisambaa mpaka kwenye figo huweza kuwa na madhara zaidi.

Aidha, maambukizi ya njia ya mkojo yanaweza kumpata yeyote, wakati wowote bila kujali jinsia na umri, lakini kwa kiasi kikubwa maambukizi haya hutokea sana kwa jinsia ya kike kutokana na maumbile yao.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa na National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK) walieleza kuwa nakadiriwa kuwa kila wanawake watano kuna mmoja anasumbuliwa na maambukizi ya njia ya mkojo yanayojirudia mara kwa mara.

Mambo ambayo huchangia tatizo hili

Aina ya Maisha
Kuna aina ya maisha ambayo yanaweza kukufanya uwe kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi sugu ya njia ya mkojo kwa urahisi. Kwa mfano mkojo unaobaki kwenye kibofu huongeza uwezekano wa bacteria kuzaliana na kusababisha maambukizi.

Pia tatizo hili huweza kuchangiwa na mwanamke anapobadili muundo wa kinga ndani ya uke wake kwa kutumia vitu vyenye kemikali kuosha uke wake, zinazoua bacteria walinzi wa kwenye uke, kama sabuni, marashi n.k. Haya yote huweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi sugu ya njia ya mkojo.

Namna ya kujikinga na maambukizi ya njia ya mkojo ya mara kwa mara

Kutokaa na mkojo kwa mda mrefu, hivyo ni vyema ukakojoa mara nyingi uwezavyo muda wowote unapojihisi kukojoa.

Kunywa maji mengi ili kusafisha bakteria kwenye njia ya mkojo.

Pendelea kuvaa nguo za ndani zenye asili ya pamba na uepuke kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

Tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment