Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 22 November 2016

Mambo manne ambayo ukiendelea nayo yatakufanya uendelee kusongwa na mawazo


Zipo sababu kadhaa ambazo huchangia mtu kuingia kwenye msongo ikiwa ni pamoja na kundamwa na shida, matatizo, dhiki.

Hali ya msongo mawazo inapokithiri ndipo mntu huanza kukosa uwezo wa kufikiri vizuri na mwishowe akili yake hushindwa kufanya kazi vizuri.

Msongo unasababishwa na vitu vingi vinavyoweza kumtokea mtu katika maisha yake.Sababu kubwa za msongo ni hizi zifuatazo; 

1. Kazi nyingi zisizomalizika kwa muda uliopangwa. 

2. Matatizo ya familia kama vile ukosefu wa pesa, chakula, ada za watoto, kuuguliwa na wanafamilia n.k

3. Kuishi maisha mabaya kama vile kula ovyo, kuvuta sigara, kuingia katika makundi mabaya kama njia ya kusahau matatizo kumbe ndio kuzidisha matatizo hayo, kujibebesha majukumu, ugomvi nyumbani na kazini husababisha mawazo mengi pia.

4. Kutokukubali matokeo ya mambo katika maisha yako kama vile mtu akiwa anakosa nafasi ya kazi hupatwa na fikra na unyonge mwingi.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment